TEHRAN, Iran
WAZIRI wa Mambo ya Nje ya Iran, Abbas Araghchi, ameitaka Marekani kuacha kusitishia nchi yake akisema vitisho pekee havitoshi.
Hivi karibuni, Rais wa Marekani, Donald Trump, aliibuka na kusema utawala wake utaingilia kati endapo mauaji ya waandamanaji yataendelea nchini Iran.
Kwa wiki kadhaa sasa, raia wa Iran wamekuwa kwenye mandamano ya kushinikiza Serikali kujiuzulu kutokana na kushindwa kushughulikia matatizo ya kiuchumi.
Huku taarifa za polisi kutumia risasi za moto dhidi ya waandamanaji, ndipo Rais Trump aliposema hataona shida kuagiza wanajeshi wake kuingia Iran ili kuwatetea raia.
Akijibu kauli hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Araghchi, amesema jeshi la nchi hiyo liko tayari kwa hatua yoyote watakayoichukua Marekani.
“Iran haitokubalia na itapinga kwa nguvu zote kuingiliwa kwa namna yoyote katika mambo yake ya ndani,” amesema.


