9.8 C
New York

Asafiri kwa baiskeli akiifuata AFCON

Published:

RABAT, Morocco

ILIKUWA ni safari ya umbali mrefu wa kilometa 3,000 akitoka Paris, Ufaransa, hadi nchini Morocco kuzifuata fainali za Mataifa ya Afrika za mwaka huu (AFCON 2025).

Akijitaja kuwa ni shabiki wa timu ya taifa ya Morocco, Ismail Skira alitimiza ndoto yake ya kuiwahi mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji hao na Comoro iliyochezwa Desemba 21.

Akitokea Paris, ilimchukua Skira wiki nne kwa safari ya baiskeli kufika mjini Agadir, Kusini mwa Morocco, ambako ndiko ilikochezwa mechi hiyo.

Skira aliyezaliwa Morocco na kuishi Paris tangu akiwa na umri wa miaka 21, anasema ndoto za kusafiria kwa baiskeli ilianza tangu mwaka 2024.

“Nilipokuwa kwenye fainali za AFCON mwaka 2024 nchini Ivory Coast, mashabiki walikuwa wakiimba nyimbo za kuzisapoti timu zao za taifa.

“Nilisikia wengine walikuja kwa ndege, magari, na baadhi kwa baiskeli, huku wengine wakija kwa miguu. Nilichagua baiskeli,” anasema Skira mwenye umri wa miaka 59.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img