Na mwandishi wetu, Gazetini
KWA mujibu wa Wikipedia, bado umri wa kuanza kupiga kura kwa mataifa mengi duniani ni miaka 18, ingawa kwa baadhi ya maeneo kuna tofauti kidogo.
Takwimu zinaonesha kuwa bado mataifa 202 duniani yanatambua umri huo kisheria kuwa ndiyo sahihi kwa raia kuanza kupiga kura.
Aidha, mataifa mengine 10 yanabaki na sheria ya kuruhusu miaka 16 kuwa umri sahihi wa kuanza kupiga kura.
Mataifa hayo ni pamoja na Brazil, Austria, Ecuador, Cuba, Nicaragua na Ujerumani kwa baadhi ya majimbo, umri huo huruhusiwa katika chaguzi ndogo.
Uingereza nayo imewasilisha mabadiliko ya sheria za uchaguzi ili kuruhusu umri wa miaka 16 kuwa mwanzo wa raia wake kuanza kupiga kura. Kwa sasa, ni miaka 18.
Kwa upande mwingine, kwa takwimu za sasa, ni mataifa manne pekee duniani yamebaki kuutambua umri wa kuanzia miaka 17 kuwa ni sahihi kuanza kupiga kura.
Ni kama ilivyo kwa Scotland na Wales, ambao raia ana haki ya kupiga kura akiwa na umri wa kuanzia miaka 16 na 17.
Hata hivyo, kwa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kwa mwanachi kuruhusiwa kisheria kupiga kura, basi anapaswa kuwa na umri wa kuanzia miaka 25.


