9.8 C
New York

Simulizi ya AFCON (4): Ebola yatikisa, Morocco yajitoa

Published:

RABAT, Morocco

HISTORIA inaturudisha mwaka 2015. Morocco ikiwa inatarajiwa kuwa mwenyeji, iliomba kuhairisha michuano hiyo kutokana na hofu ya kuingiziwa maambukizi ya ugonjwa wa Ebola.

Ni kipindi ambacho ugonjwa huo ulikuwa umeshika kasi katika mataifa mengi ya Ukanda wa Afrika ya Magharibi.

Hata hivyo, Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) lilikataa ombi la Morocco ikiwa imebaki miezi miwili tu kabla ya AFCON kuanza.

Haikuishia hapo. CAF iliiadhibu Morocco kwa kuinyima nafasi ya kushiriki mashindano hayo makubwa zaidi kwa ngazi ya timu za taifa barani Afrika.

Baada ya mataifa matano kukataa kuchukua nafasi ya Morocco, Guinea ya Ikweta ilikubali kuwa mwenyeji. Ivory Coast ilitwaa ubingwa wa penalti 9-8 dhidi ya Ghana katika mchezo wa fainali.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img