9.8 C
New York

Simulizi za AFCON (1): Drogba na waasi wa Ivory Coast

Published:

ABIDJAN, Ivory Coast

AKIWA kwenye kiwango cha juu na mafanikio makubwa ya soka, wakati huo akiitumikia Chelsea, Didier Drogba, alijitosa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyokuwa ikiendelea nchini kwao, Ivory Coast.

Kama kuzungumza haitoshi, Drogba alifikia hatua ya kupiga magoti akiwa kwenye mahojiano ya televisheni. Aliwaomba waasi kuweka silaha chini ili amani irejee Ivory Coast.

Ni vita iliyoanza mwaka 2002. Hatimaye, pande zote mbili, kwa maana ya wanajeshi wa Serikali na waasi, wakaweka silaha chini mwaka 2007.

Baada ya utulivu wa muda kurejea, Drogba aliomba mechi yao ya kufuzu fainali za AFCON za mwaka 2008 ikachezwe Bouake, Mji ambao ndiyo uliokuwa kambi ya waasi.

Ivory Coast ilipofuzu, Drogba akawageukia tena wachezaji wenzake akitwaambia kutwaa taji la AFCON kungerejesha zaidi hali ya utulivu na kuliunganisha tena Taifa lao.

Hata hivyo, Drogba hakufanikiwa kutimiza ndoto hiyo. Alishindwa kutwaa taji hilo, licha ya kufika mara mbili hatua ya fainali na kufungwa kwa penalti.

Lakini, mara zote Drogba amekuwa akisisitiza kuwa ubingwa wa AFCON si kitu, na badala yake anajivunia kurejesha hali ya amani nchini Ivory Coast.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img