11.2 C
New York

Mwanasiasa upinzani afariki akiwa kizuizini

Published:

YOUNDE, Cameroon

TAHARUKI imetawala nchini Cameroon baada ya mwanasiasa mkongwe wa upinzani, Anicet Ekane, kufariki akiwa anashikiliwa na vyombo vya dola, ikiwa ni wiki tano zimepita tangu alipokamatwa.

Ekane aliyefariki akiwa na umri wa miaka 74, alikuwa sehemu ya viongozi wa muungano wa vyama vya upinzani vilivyomuunga mkono Issa Tchiroma Bakary aliyewania urais katika Uchaguzi wa Oktoba, mwaka huu.
Tchiroma Bakary, kama itakumbukwa, alijitangaza mshindi wa kiti cha urais hata kabla ya Tume ya Uchaguzi kumtangaza Rais Paul Biya.

Tangu wakati huo, Tchiroma Bakary amekuwa akiishi Gambia, akihofia utawala wa Biya, ambaye ana umri wa miaka 92 na huu ni muhula wake wa tisa madarakani.

Hakuna taarifa rasmi huu ya chanzo cha kifo cha mkongwe huyo wa siasa za upinzani, ingawa chama chake kimeitupia lawama Serikali kikidai alinyimwa haki ya kupata matibabu.

Kupitia Msemaji wa Chama chake cha African Movement for New Independence and Democracy (Manidem), Ekane alifariki akiwa katika Hospitali ya jeshi na alipelekwa hapo baada ya afya yake kudorora mno.

Hata hivyo, ni madai ambayo yamepingwa vikali na Msemaji wa Serikali, Rene Emmanuel Sadi, akisema Ekane alipatiwa huduma zote za matibabu kwa kipindi chote alichokuwa gerezani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img