3.9 C
New York

Yanga haitanii, yafikisha pointi nne CAF

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini
KATIKA mchezo wa jana, JS Kabylie ikiwa nyumbani ilimazilishwa suluhu na Yanga, ukiwa ni mchezo wa Kundi B msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kabylie ilihitaji ushindi ili walau kurejesha matumaini baada ya kufungwa mabao 4-1 na Al Ahly katika mchezo wa kwanza wa michuano hiyo ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).
Hivyo, Al Ahly itaendelea kubaki kileleni mwa msimamo ikiwa na pointi nne, sawa na Yanga inayoshika nafasi ya pili.
AS FAR, ambayo ilifungwa bao 1-0 na Yanga katika mchezo wa kwanza, jana ikiwa nyumbani nchini Morocco ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Al Ahly.
Hivyo, AS FAR inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi moja, sawa na JS Kabylie inayoburuza mkia.
Katika raund inayofuata, Yanga itamenyana na Al Ahly (Januari 23, mwakani) wakati AS FAR itamenyana na JS Kabylie.
‘Timu ya Wananchi’ sasa inarejesha makali yake Ligi Kuu Bara, ambapo itashuka dimbani Desemba 2, mwaka huu, kwa mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img