20 C
New York

Singida Fountain Gate kuzindukia kwa Dodoma?

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini
UKITUPA macho kwenye msimamo, Singida Fountain Gate iko mkiani ikiwa imezibeba timu zingine 19 zinazoshiriki msimu huu wa Ligi Kuu Bara.
Iko hivi; Singida haijafanikiwa kuonja ushindi wala kuambulia sare na badala yake imefungwa mechi zote tatu ilizoshuka dimbani.
Mbaya zaidi kwa wakali hao wa mkoani Singida, ndiyo timu pekee ambayo haijafunga bao na imeruhusu mabao mengi zaidi (6).
Ilifungua msimu kwa kichapo cha bao bao 1-0 dhidi ya Mbeya City, ikafungwa mabao 3-0 na Simba SC, kisha ikalazwa mabao 2-0 na Mtibwa Sugar.
Hivyo, katika mchezo ujao wa Ijumaa ya Oktoba 17, mwaka huu, Singida watakuwa nyumbani kuwakaribisha Dodoma FC.
Hii itakuwa mechi ya pili kwa Singida kucheza nyumbani, ikikumbukwa kuwa ilifungwa mbele ya mashabiki wake katika ile ya ufunguzi wa msimu dhidi ya Mbeya City.
Kwa upande wake, Dodoma FC si ya kubeza msimu huu. Katika mechi tatu, imeshinda moja, sare moja, imefungwa moja na inashika nafasi ya sita katika msimamo ikiwa na pointi nne.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img