20 C
New York

Mechi 42, mabao 36 Ligi Kuu Bara 2025-26

Published:

Na Hassan Mwasha
KABLA ya mapumziko ya kupisha mechi za timu za taifa zilizo kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), msimu huu wa Ligi Kuu Bara ulishafikisha mechi 42 za raundi ya kwanza.
Kati ya timu 20, ni sita pekee zilizocheza mechi mbili kila moja, ambazo ni Simba, Singida Big Stars, Yanga, Azam, Mtibwa Sugar na Tabora United.
Hivyo basi, kwa hesabu zilivyo, timu zingine 14 zilizobaki zimeshashuka dimbani mara tatu kila moja.
Kwa upande mwingine, mechi 42 zilizokwishachezwa zimeshuhudia mabao ya kufunga yakiwa ni 36 kufikia hatua hii ya msimu.
Katika mabao hayo, Simba imechangia mengi sita, ikifuatiwa na JKT Tanzania (4), Dodoma FC (4), Yanga (3) na Azam FC (3).
Pia, katika mechi 42, yameshuhudiwa mabao ya kufungwa 36. Singida Big Stars ndiyo timu iliyoruhusu mabao mengi zaidi (6) kufikia sasa.
Timu zingine zenye idadi kubwa ya mabao ya kufungwa ni Namungo (4), Pamba Jiji (4), Coastal Union (4), JKT Tanzania (3), na Dodoma FC (3).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img