20 C
New York

Mbeya City kwa Yanga, Pamba Jiji na Tabora

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini
KUFIKIA hatua hii ya msimu wa 2025-26 wa Ligi Kuu Bara, zimeshashuhudiwa sare 12 lakini suluhu (0-0) ni mbili pekee, kwa mujibu wa takwimu.
Kwamba ni mechi mbili pekee zilizoshuhudia dakika 90 zikimalizika kwa timu zote mbili zikiondoka uwanjani zikiwa hazijapasia nyavu.
Iko hivi; unaikumbuka mechi kati ya Mbeya City na Yanga? Ilichezwa Septemba 30, mwaka huu, katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na dakika 90 zilimalizika kwa suluhu.
Kama itakumbukwa, huo ulikuwa ni mchezo wa pili wa Yanga baada ya ule wa kwanza walioibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Pamba Jiji.
Mechi nyingine iliyoshuhudia dakika 90 zikimalizika bila bao ni ile iliyozikutanisha Pamba jiji na Tabora United wikiendi ya Septemba 28, mwaka huu, ambayo ilichezwa katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img