20 C
New York

Gamondi mtu wa kazi Singida Black Stars

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini
UKIACHA Simba, Singida Black Stars ndiyo timu pekee ambayo si tu haijafungwa, bali pia imeshinda mechi zote ilizoshuka dimbani msimu huu wa Ligi Kuu Bara.
Chini ya kocha wa zamani wa Yanga, Miguel Angel Gamondi, Singida BS wamekusanya pointi sita katika mechi zao mbili walizokutana na Mashujaa FC na KMC.
Ikumbukwe, Singida walifungua pazia na KMC katika mchezo waliokuwa ugenini jijini Dar es Salaam, ambapo waliondoka na ushindi wa bao 1-0.
Mechi yao ya pili iliwakutanisha na Mashujaa mjini Singida na vijana wa Gamondi walizoa tena pointi tatu kwa ushindi wa aina hiyo (1-0).
Kutokana na ushiriki wake kwenye michuano ya kimataifa, Singida BS watarejea Ligi Kuu Oktoba 30, mwaka huu, kwa mchezo dhidi ya matajiri wa Chamazi, Azam FC.
Ni baada ya kucheza mechi mbili (nyumbani na ugenini) dhidi ya Flambeau du Centre ya Burundi katika hatua ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img