LONDON, Uingereza
IMERIPOTIWA kuwa klabu za England, Arsenal na Liverpool, kila moja inajaribu kuinasa huduma ya mshambuliaji wa Real Madrid raia wa Brazil, Vinicius Jr.
Vinicius atamaliza mkataba wake mwaka 2027 lakini kwa sasa hakua makubaliano aliyofikia na Madrid juu ya kuongeza mwingine baada ya hapo.
Kwa mujibu wa ripoti, Madrid wanataka asaini mkataba mpya na ofa yao mezani ni Pauni milioni 17.5 lakini Vinicius amegoma na kuwaambia wafike Pauni milioni 26.
Vyanzo vya habari barani Ulaya vimeeleza kuwa Arsenal na Liverpool ziko mstari wa mbele kufuatilia kinachoendelea kati ya Madrid na mchezaji huyo.
Hata hivyo, inaeleweka kuwa hizo ni tarifa tu lakini hakuna klabu iliyopeleka ofa rasmi kwa mabosi wa Santiago Bernabeu.
Arsenal wameimarisha safu ya ushambuliaji kwa kuwasajili Viktor Gyokeres na Eberechi Eze lakini ujio wa Vinicius utaliongezea makali zaidi eneo hilo.
Liverpool, kwa upande wao, waliwaongeza kikosini Florian Wirtz, Hugo Ekitike na Alexander Isak lakini Vinicius anaweza kuwa mchezaji sahihi zaidi kusajiliwa endapo Mohamed Salah ataondoka.
Published:


