13.9 C
New York

Palestina yaiita mezani Israel kumaliza vita

Published:

JERUSALEM, Palestina
RAIS wa Palestina, Mahmoud Abbas, amesema yuko tayari kushiriki katika mpango wowote wa kutafuta suluhu kati yao na Israel.
Abbas ameyasema hayo kupitia video yake kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Ikumbukwe, Abbas mwenye umri wa miaka 89, alishindwa kushiriki moja kwa moja baada ya Marekani kumzuia kuingia jijini New York unakofanyika Mkutano huo.
Aidha, ametumia nafasi hiyo ya mazungumzo ya video kuyaomba mataifa mengine kufuata nyayo za Ufaransa na Uingereza kwa kuitambua Palestina kama taifa huru.
Ni katika video hiyo pia, amesikika akisema mashambulizi yanayofanywa na Israel kwa wananachi Gazza ni ukatili mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika karne ya 20 na 21.
Hata hivyo, Abbas amekiri kutokuunga mkono shambulizi kubwa lililofanywa na Kundi la Hamas dhidi ya Israel mwaka 2023.
Shambulizi hilo la Oktoba 7 liliua watu 1,200, huku wengine 251 wakitekwa na Kundi hilo la Palestina.
Tangu hapo, raia wa Palestina 65,502, wakiwamo wanawake na Watoto, wameuawa na wanajeshi wa Israel katika mashambulizi kadhaa huko Gaza.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img