LONDON, Uingereza
KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, atamkosa kwa wiki sita hadi nane winga wake mpya, Noni Madueke, baada ya nyota huyo kupata majeraha ya goti.
Taarifa zinaeleza kuwa Madueke aliyesajiliwa akitokea Chelsea, aliumia katika mchezo wa sare ya bao 1-1 dhidi ya Manchester City wikiendi iliyopita.
Ni kwa maana hiyo basi, Madueke mwenye umri wa miaka 23 atakuwa fiti kufikia Novemba, mwaka huu.
Aidha, si tu ni pigo kwa Arsenal, pia timu ya taifa ya England itamkosa katika mechi mbili zijazo dhidi ya Wales na Latvia.
Hata hivyo, habari njema kwa mashabiki wa Arsenal ni kwamba staa huyo atakuwa fiti kuikabili Tottenham katika ‘derby’ ya Novemba 23.
Published:


