13.4 C
New York

Neville amkosoa Arteta kisa sare ya City

Published:

MANCHESTER, Uingereza
MKONGWE wa Ligi Kuu ya England, Gary Neville, amemtaka Mikel Arteta kuachana na mbinu zake.
Kauli ya beki huyo wa zamani wa Manchester United imekuja baada ya Arsenal kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Manchester City katika mchezo wa jana.
Katika mchezo huo wa Ligi Kuu, Washika Bunduki wa London walilazimika kusubiri hadi dakika za majeruhi kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Gabriel Martinelli.
Akizungumzia mechi hiyo, Neville mwenye umri wa miaka 50 alisema tatizo kubwa la Arteta ni kutegemea mipira ya kutenga katika kupata ushindi.
“[Pep] Guardiola alishamfahamu Arsenal kuwa ni kocha anayetegemea mbinu za aina moja.
“Mipira ya kutenga ndiyo silaha ya mabao mengi wanayofunga (Arsenal).”
Mbali ya hilo, Neville alikosoa namna Arteta alivyoteua kikosi cha kuikabili Man City katika mchezo huo uliochezwa Etihad.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img