13.9 C
New York

Obama amvaa Trump, aionya Marekani

Published:

WASHINGTON DC, Marekani
RAIS wa zamani wa Marekani, Barack Obama, amesema kwa sasa nchi hiyo inapitia wakati mgumu kisiasa, labda kuliko nyakati zote kuwahi kutokea.
Obama ameyasema hayo wakati akilaani vikali mauaji ya mwanasiasa wa upinzani, Charlie Kirk, ambaye alipigwa risasi hivi karibuni.
Kirk aliyefariki akiwa na umri wa miaka 31, alipigwa risasi akiwa anazungumza katika Chuo Kikuu cha Utah Valley mjini Orem.
Akizungumza katika Jimbo la Pennsylvania juzi, Obama alikosoa kauli za Rais Donald Trump dhidi ya wanasiasa wa upinzani.
Alisema: “Nafikiri kwa sasa, hali ni mbaya na ni kazi ya Rais kuwaleta watu pamoja. Muhimu ni kuheshimu hata wale ambao hatukubaliani nao.”
Kwa upande wake, Ikulu ya Marekani imemjibu Obama kwa kumwita ‘mbunifu wa siasa za kisasa’.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img