11.2 C
New York

Onana rasmi ajiunga na Trabzonspor

Published:

ISTANBUL, Uturuki
MLINDA mlango wa kimataifa wa Cameroon, Andre Onana, amejiunga na Trabzonspor ya Uturuki akitokea Manchester United kwa mkopo wa msimu mmoja.
Usajili huo ulikamilishwa muda mfupi kabla ya dirisha la usajili la Uturuki kufungwa usiku wa kuamkia leo.
“Tunapenda kumtakia kila la kheri Andre,” ilieleza taarifa ya klabu yake ya Man United.
Onana ameondoka Old Trafford akiwa amecheza mechi moja pekee msimu huu, ambayo hata hivyo walifungwa na Grimsby Town na kutolewa katika michuano ya Carabao.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29, alitua Man United mwaka 2023 akitokea Inter Milan, usajili huo ukilenga kuziba pengo la David de Gea.
Ameondoka Old Trafford akiwa amecheza mechi 102 na alikuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa taji la FA mwaka 2024.
Kuondoka kwake kunakuja zikiwa ni siku chache tu zimepita tangu Man United ilipomsajili kipa raia wa Ubelgiji, Senne Lammens.
Kwa sasa, kocha Ruben Amorim, ambaye keshokutwa atakwaana na Manchester City, anabaki na Lammens, Altay Bayindir na Tom Heaton katika eneo la langoni.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img