13.1 C
New York

Mbappe aifikia rekodi ya mkongwe Ufaransa

Published:

PARIS, Ufaransa
NAHODHA wa timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe, amefikisha mabao 51 akiwa na kikosi hicho, akiifikia rekodi ya Thierry Henry.
Mbappe aliandika historia hiyo katika mchezo wa jana dhidi ya Ukraine, ambapo Ufaransa ilipata ushindi wa mabao 2-0.
Kwa sasa, nyota huyo wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 26 amebakiza mabao sita pekee kumfikia Olivier Giroud, ambaye ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Ufaransa.
“Hongera kwa Titi [Henry] lakini sasa nataka kuivunja rekodi yake,” alisema Mbappe.
“Ni heshima kubwa kufikia rekodi za wachezaji wakubwa kama Henry, hakuna asiyefahamu alivyo mtu muhimu kwetu sisi Wafaransa na washambuliaji kwa ujumla.
Henry alikuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 1998 akiwa na umri wa miaka 20.
Kwa upande wake, Mbappe aliiongoza timu hiyo kuwa mabingwa wa dunia akiwa na miaka 19, fainali zilizofanyika mwaka 2018 nchini Urusi.
Hata hivyo, si tu Giroud amewazidi mabao, bali pia ndiye mchezaji mwenye mechi nyingi (137) katika historia ya timu ya taifa ya Ufaransa.
Ikumbukwe, Henry alitangaza kustaafu akiwa amecheza mechi 123, wakati Mbappe ameshashuka dimbani mara 90.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img