11.2 C
New York

Vazquez aondoka La Liga, atua Leverkusen

Published:

MADRID, Hispania
WINGA wa kimataifa wa Hispania, Lucas Vazquez, ametimka Real Madrid na kujiunga na Bayer Leverkusen akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake Santiago Bernabeu.
Vazquez (34), ameondoka Madrid akiwa ametwaa mataji matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na manne ya Ligi Kuu (La Liga).
Nyota huyo amesaini mkataba wa miaka miwili na Leverkusen inayonolewa na kocha wa zamani wa Manchester United, Erik ten Hag.
Akizungumzia usajili huo, Vazquez alisema kocha wa Madrid, Xabi Alonso, alihusika kumshawishi kujiunga na Leverkusen.
Alitokea katika ‘academy’ ya Madrid na kucheza mechi yake ya kwanza ya timu ya wakubwa mwaka 2015.
Anaondoka Bernabeu akiwa amecheza mechi 402, pia akiwa na jumla ya mataji 20, yakiwamo matatu ya Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img