9.8 C
New York

Galatasaray watua England kumfuata Bissouma

Published:

LONDON, Uingereza
WAKONGWE wa Ligi Kuu ya Uturuki, Galatasaray, wameripotiwa kuitaka saini ya kiungo wa ulinzi wa Tottenham, Yves Bissouma.
Nyota huyo raia wa Mali hajacheza mechi yoyote msimu huu, akitajwa kuponzwa na vitendo vya utovu wa nidhamu.
Bissouma (28), alitua Spurs akitokea Brighton mwaka 2022, usajili huo ukigharimu kitita cha Pauni milioni 25.
Kwa miaka mitatu klabuni hapo, amecheza mechi 100, ikiwamo iliyowapa ubingwa wa Ligi ya Europa msimu uliopita baada ya kuifunga Manchester United bao 1-0.
Nafasi ya Bissouma kuanza kikosini imeonekana kupata upinzani, hasa baada ya Tottenham kumsajili Joao Palhinha.
Palhinha, raia wa Ureno aliyetua kwa mkopo akitokea Bayern Munich, alifunga bao katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester City.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img