LONDON, Uingereza
KLABU ya Nottingham Forest iko mbioni kumfuta kazi kocha Nuno Espirito Santo, wakati huo pia ikimpigia hesabu Brendan Rodgers anayeinoa Celtic kwa sasa.
Rodgers (52), ni kipenzi cha mmiliki wa Nottingham, Evangelos Marinakis, ambaye uhusiano wake na Nuno umetajwa kuyumba katika siku za hivi karibuni.
Rodgers, kocha wa zamani wa Liverpool na Leicester City, ameingia mwaka wa mwisho katika mkataba wake na Celtic ya Scotland.
Nuno (51), ameingia kwenye matatizo na tajiri Marinakis baada ya kocha huyo kukosoa uamuzi wa klabu hiyo kutosajili wachezaji kipindi hiki cha majira ya kiangazi.
Ukiacha jina la Rodgers, pia kocha aliyeondoka Tottenham, Ange Postecoglou, naye anahusishwa na kibarua cha kuinoa Nottingham.
Awali, pia zilikuwepo tetesi kuwa Marinakis anaweza ‘kuvunja kibubu’ na kumuajiri kocha wa Fenerbahce, Jose Mourinho.
Published:


