13.1 C
New York

Ajali yaua waliotoka msibani

Published:

NAIROBI, Kenya

WATU 25 waliokuwa wakirejea kutoka msibani wamefariki baada ya basi walilokuwa wamepanda kupata ajali huko Magharibi mwa Kenya. Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, tukio hilo limetokea katika barabara ya Kisumu-Kakamega, ambayo imekuwa chanzo kikubwa cha ajali.

Taarifa inaeleza zaidi kuwa basi hilo lilikuwa linarejea Nyakach likitokea msibani maeneo ya Nyahera.
Kwa upande mwingine, polisi wameeleza kuwa kuwa mbali ya waliofariki, ajali hiyo imesababisha watu 20 kujeruhiwa.

Hata hivyo, kwa kile kilichoelezwa na polisi, bado chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika, licha ya kwamba uchunguzi unaendelea.

Wakati huo huo, Wizara ya Afya ya Kenya imeeleza kusikitishwa na tukio hilo, pia ikiomba uchunguzi wa haraka juu ya chanzo chake.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img