24.2 C
New York

Nabi apata majanga, arudi Tunisia

Published:

PRETORIA, Afrika Kusini
KOCHA wa Kaizer Chiefs, Nasreddine Nabi, atakosa mechi ya ufunguzi ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini baada ya mkewe kupata ajali ya gari.
Nabi atakosekana kwenye benchi kesho, wakati vijana wake wa Kaizer watakapoivaa Stellenbosch FC katika Uwanja wa Athlone mjini Cape Town.
Taarifa iliyoripotiwa moja kwa moja na Kaizer imeeleza kuwa Nabi amerejea nyumbani, Tunisia.
“Tunasikitika kuwajulisha mashabiki wetu kwamba kocha Nasreddine Nabi hatasafiri na timu kwenda Cape Town kwa ajili ya mchezo wa ufunguzi wa msimu dhidi ya Stellenbosch FC,” ilieleza taarifa ya klabu hiyo.
Kwa kukosekana kwake, kocha msaidizi, Khalil Ben Youssef, atashirikiana na mwenzake, Cedric Kaze, kuiongoza Kaizer katika mchezo huo.
“Kaizer Chiefs tunapenda kuwapa pole Nabi na familia yake katika kipindi hiki kigumu…” ilieleza zaidi taarifa hiyo.
Hata hivyo, taarifa ya Kaizer haikuweka wazi siku ambayo kocha huyo atarejea Afrika Kusini kuungana na timu.

Related articles

Recent articles