24.2 C
New York

Frimpong kuziba pengo la Salah

Published:

MERSEYSIDE, England
KOCHA wa Liverpool, Arne Slot, amefichua kuwa atamtumia mchezaji wake mpya, Jeremie Frimpong, katika eneo analocheza staa wa timu hiyo, Mohamed Salah.
Salah raia wa Misri, atakosa mechi takribani sita za Ligi Kuu ya England kuanzia Desemba 21, mwaka huu, hadi Januari 18, mwakani, kutokana na fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON).
Kwa mujibu wa Slot, Frimpong aliyegharimu Pauni milioni 29 akitokea Bayer Leverkusen ni mzuri pia akicheza winga wa kulia, licha ya kwmba alisajiliwa kuziba pengo la beki wa kulia, Trent Alexander-Arnold.
“Tulifikiria kuhusu hilo (Salah kwenda AFCON). Tulimsajili Jeremie kwa kuwa tunaamini anaweza kucheza kama beki wa pembeni, pia anaweza kuwa winga wa kulia,” alisema Slot.
“Usajili wa Jeremie Frimpong ulikuwa na maana kubwa, ikiwamo ya kuziba pengo la Mo. Nina njia nyingi za kuziba pengo la Mo, ikiwamo kumtumia Jeremie.”

Related articles

Recent articles