25.2 C
New York

CAF yaipanga Simba ya tano, Yanga ya 12 viwango vya ubora Afrika

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Klabu ya Simba SC imepanda hadi nafasi ya tano katika viwango vipya vya ubora vya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), huku watani wao wa jadi Yanga SC wakishikilia nafasi ya 12.

Kwa mujibu wa chati rasmi ya CAF iliyotolewa leo, Simba imekusanya pointi 48 kutokana na mafanikio yake katika mashindano ya klabu ya CAF ndani ya misimu mitano iliyopita, ikiwamo kufika fainali mara moja na robo fainali mara nne.

Kwa upande wa Yanga, imekusanya pointi 34 baada ya kufika fainali mara moja, robo fainali mara moja, na hatua ya makundi mara moja ndani ya kipindi hicho hicho.

Viwango hivi vya ubora vitatumika katika upangaji wa droo ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika kwa msimu ujao, itakayochezeshwa kesho Jumamosi, Agosti 9, 2025 jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Mabingwa watetezi wa CAF Champions League, Al Ahly ya Misri, inaongoza katika chati hiyo ya CAF, ikifuatiwa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, wakati Esperance ya Tunisia inashika nafasi ya tatu.

Nafasi nyingine kumi bora zimepangwa kama ifuatavyo:
4. RS Berkane (Morocco)
5. Simba SC (Tanzania)
6. Pyramids FC (Misri)
7. Zamalek (Misri)
8. Wydad AC (Morocco)
9. USM Alger (Algeria)
10. CR Belouizdad (Algeria), 11. Al Hilal na 12. Yanga.

Katika droo ya kesho, ni timu mbili pekee—Al Ahly na Mamelodi Sundowns—zitakazoanza moja kwa moja hatua ya makundi, kutokana na viwango vyao vya juu na historia yao ya karibuni katika mashindano ya kimataifa.

Timu hizo mbili ziliiwakilisha Afrika kwenye Fainali za Kombe la Dunia la Klabu zilizofanyika Marekani, ambako Chelsea iliibuka bingwa. Timu nyingine za Afrika zilizoshiriki mashindano hayo ni Esperance ya Tunisia na Wydad AC ya Morocco.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img