LONDON, England
MWENYEKITI wa Tottenham, Daniel Levy, amefichua kuwa mkataba wa Harry Kane una kipengele kinachowaruhusu kumsajili kwa mara nyingine. Kane, nahodha wa timu ya taifa ya England, aliondoka Spurs na kutua Bayern Munich mwaka 2023, usajili huo ukigharimu Pauni milioni 86.
Spurs waliwahi kufanya hivyo kwa Gareth Bale, ambaye alikwenda Real Madrid kwa Pauni milioni 85, kabla ya kurejea kwa mkopo hapo baadaye. Kwa mujibu wa LevyLevy, mkataba wa Kane una kipengele kinachowapa nafasi ya kumrejesha kwa Pauni milioni 67.
Hata hivyo, Kane mwenye umri wa miaka 32 amekuwa akisisitiza kuwa haoni kama kuna uwezekano wa kuondoka Bayern hivi karibuni.


