13.9 C
New York

Ndege ya Air India yaanguka na kuwaka moto

Published:

Na Mwandishi Wetu

Ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la  India ‘Air India’  iliyokuwa inatokea nchini India kwenda London nchini Uingereza imeanguka na kuwaka moto leo Juni 12,2025 katika eneo la Ahmedabad India muda mfupi baada ya kupaa ikiwa na watu 242.

Kwa mujibu wa taarifa za mamlaka nchini India zimesema ndege hiyo ikuwa imebeba  idadi hiyo ya watu   ambapo  abiria 169 ni raia wa India,  raia wa  53 Uingereza, Wareno saba na raia wa Canada mmoja, huku wafanyakazi wa ndege hiyo  ni 12.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi  kupitia mtandao wake wa kijamii wa X, amesema ameshtushwa sana na ajali hiyo ya ndege.

“Ajali ya Ahmedabad imetushtua na kutuhuzunisha. Haielezeki jinsi inavyovunja moyo, amesema Modi katika ujumbe huo alioandika.

Mtandao wa kufuatilia safari za ndege wa Flightradar24 umesema ndege hiyo ilikuwa aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, mojawapo ya ndege za kisasa zaidi zinazotumika.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img