1.7 C
New York

Visual| Tunachofahamu kuhusu chanjo ya Uviko-19 Tanzania

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Hadi kufikia Julai 18, 2022 jumla ya wananchi milioni 11.5 sawa na asilimia 37 ya watu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea wamepata chanjo kamili ya Uviko-19 nchini Tanzania.

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati akizungumza Julai 20, katika kikao cha Viongozi wa dini wa Mkoa wa Tanga ikiwa ni mkakati wa uhamasishaji wa kuongeza kasi ya kuchanja nchini.

“Tumeshachanja watu milioni 11.5 wamepata kinga kamili kati ya watu milioni 30.7 ambao tumewalenga, sasa hivi imethibitika pasi na shaka kwamba chanjo ndio njia pekee ya uhakika inayoweza kupunguza makali ya Uviko-19 na ili tuweze kutengeneza kinga ya jamii, dunia imejiwekea malengo angalau tuweze kuchanja asilimia 70 ya watu wote duniani,” amebainisha Ummy.

“Tumeshachanja watu milioni 11.5 wamepata kinga kamili kati ya watu milioni 30.7 ambao tumewalenga, sasa hivi imethibitika pasi na shaka kwamba chanjo ndio njia pekee ya uhakika inayoweza kupunguza makali ya Uviko-19 na ili tuweze kutengeneza kinga ya jamii, dunia imejiwekea malengo angalau tuweze kuchanja asilimia 70 ya watu wote duniani,”

@ummymwalimu

Aidha, Waziri Ummy amebainisha kwamba idadi hiyo imefikiwa kutokana na kampeni iliyoanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan mwaka 2021 ikiwemo huduma tembezi, kusogeza vituo vya kuchanja karibu na maeneo ya watu ambapo vituo vya kutolea chanjo vilikua 550 mwaka 2021 na kufikia vituo 7,000 mwaka 2022.

Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inatambua na itaendelea kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Taasisi za dini hapa nchini katika mapambano dhidi ya magonjwa ikiwemo ugonjwa wa Uviko-19 hivyo kikao hicho kitaleta mbinu mbalimbali za kuwafikishia wananchi.

“Tunaamani kabisa ninyi viongozi wa dini mnajihusisha kwenye mambo ya jamii mna mambo makubwa ya kutufundisha na mtatupatia mbinu na mikakati mbalimbali za kwenda kuwahamasisha wananchi, ninyi tangu ugonjwa huu kuingia nchini mmekua mnatusaidia kufikisha elimu kwa jamii kujikinga na ugonjwa huu,” amesema Waziri Ummy

Kuhusu hali ya uchanjaji kwa Mkoa wa Tanga Waziri Ummy amesema Mkoa wa Tanga ipo asilimia 22 kati ya asilimia 37 ya Kitaifa na Wilaya ya Muheza wamechanja asilimia 69 na kufuatiwa na Pangani asilimia 40, Korogwe mji 38, handeni mji 35 na Tanga jiji asilimia 26.

Zaidi angalia usanifu wetu hapo juu kuona mwenendo wa chanjo ya Uviko-19 Oktoba, mwaka 2021 hadi sasa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img