Kutoka katika Ripoti ya Shirika la Haki Elimu Tanzania ya Utafiti wa Elimu ya Msingi na Sekondari kwa wasichana ya Mwaka 2019 utafiti ulifanyika kuangalia athari anazozipata mtoto wa kike na kushindwa kujiamini au kuonekana katika kukabiliana nazo ikiwemo vishawishi vya kuanza mahusiana au kupata ujauzito.
Utafiti huo ulifanyika katika Mikoa mitano ya Tanzanai Bara ambayo ni Dar es Salaam, Lindi, Kilimanjaro, Dodoma na Tabora Halmashari za Wilaya zilizofikiwa ni 12, Kata 24, Shule 63 na wanafunzi waliohojiwa ni 1841.
Utafiti pia umezitaja sababu zinazo athiri wasichana kushindwa kujiamini na kuonekana katika utatuzi wa mambo yanayowakabili ambazo zimegawanyika katika makundi matatu, mazingira ya nyumbani ambako vijana wanaishi, mazingira ya kujifunzia na kusoma kutokua rafiki kwa msichana pamoja na tabia za kijinsia.
Katika ukurasa wa 38 Jedwali linaonesha asilimia za wasichana waliokua na wapenzi wakiwa Shule na wale walisema hawana wapenzi kwenye ngazi ya Mkoa na Wilaya ambapo unaweza kuangalia viwango hivyo kupitia usanifu wetu hapo juu.