22 C
New York

RIPOTI| Kwa mwajiriwa, ishu ni masilahi au afya?

Published:

DAR ES SALAAM, TANZANIA

KWA bahati mbaya, kipaumbele cha walio wengi huwa ni kupata nafasi ya ajira, shughuli yoyote inayoweza kumuingizia kipato.

Hivyo basi, asilimia kubwa ya wanaotafuta ajira huelekeza akili zaidi kwenye kiasi cha fedha atakacholipwa na mwajiri wake.

Ni nadra au hakuna kabisa uwezekano wa kusikia suala la afya likitajwa aidha na mwajiriwa au mwajiri.

Kwamba hata katika mazungumzo ya kuanza kazi, ‘ishu’ huwa ni masilahi na si namna bosi atavyowajibika katika ulinzi wa afya ya mwajiriwa mpya.

Kwa namna moja au nyingine, hilo hutokana na uelewa mdogo juu ya sheria zinazosimama kutetea afya ya mfanyakazi awapo eneo lake la ajira.

Kazi huua watu milioni mbili, wagonjwa milioni 300

Ieleweke kuwa Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO) lina utafiti uliobaini kuwa takribani watu milioni mbili hufariki dunia kila mwaka duniani kote kutokana na ajali au magonjwa yatokeayo kazini.

Kama hiyo haitoshi, watu zaidi ya milioni 300 huugua magonjwa waliyoyapata maeneo yao ya ajira.

Ndiyo maana, Shirika hili, ILO, lilipitisha Mkataba wa

Usalama na Afya Kazini mwaka 1981, lengo likiwa ni kuwabana mabosi waweze kubeba jukumu la kulinda afya za wafanyakazi wao.

Hali ikoje Tanzania?

Aidha, hapa nchini ipo Sheria ya Afya na Usalama Kazini ya

mwaka 2003, ambayo pamoja na Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004, zinatoa

ulinzi kwa waajiriwa wawapo kazini, kuhakikisha ‘wanatumika’ wakiwa kwenye mazingira bora na salama, ikiwamo kuwapatia vifaa vya kazi na mafunzo ya kuzilinda afya zao.

Lakini, ripoti ya mwaka huu ya Tume ya Haki za Binadamu nchini (LHRC) imebaini udhaifu mkubwa katika utekelezaji wa Sheria mbili hizi.

Ni ripoti iliyohusisha utafiti katika mikoa 15 ya Tanzania Bara na kujumuhisha biashara na makampuni 160, huku washiriki 2,600 wakitumika kutoa maoni.

Majibu ya utafiti yalionesha kwamba ni 59% pekee ya mahala pa kazi (biashara na kampuni) kulikuwa na sera ya afya na usalama kwa wafanyakazi.

Ni kama ripoti ilivyoeleza kuwa asilimia 43 ya wafanyakazi waliohojiwa na watafiti walidai kutopewa mafunzo juu ya afya na usalama kazini.

Hata wawakilishi wa kampuni na viwanda waliodai kuwa na sera ya afya na usalama kwa wafanyakazi wao, ni theluthi moja pekee walioweza kuwaonesha watafiti nakala za sera hiyo.

Katika kile kilichoonekana kuwa hatarishi kwa afya za wafanyakazi, vyoo vilionekana kutokidhi matakwa ya kisheria, licha ya washiriki wengi (78%) kudai kuridhika navyo.

Pia, kwa kuwa mwajiri analazimika kulinda afya za waajiriwa, ripoti ya mwaka huu ya LHRC imebaini kuwa bado kumekuapo na msukumo mdogo kwa waajiri kuhakikisha waajiriwa wanakuwa na vifaa vya kazi.

Ripoti hii inaonesha ukubwa wa tatizo hilo kwa kuwa ni asilimia 39 tu ya wafanyakazi waliokiri kuwa na vifaa vya kazi, ingawa watafiti walivitoa kasoro kutokana na uchakavu wake.

Juu ya tatizo hilo, Shinyanga na Geita ndiyo mikoa iliyoibua washiriki wengi waliolalamika kukosa vifaa vya kazi kwenye maeneo yao ya ajira.

Je, mwajiri wako anajali afya yako? Kama jibu ni hapana, unachukua hatua gani baada ya elimu hii iliyotokana na utafiti wa LHRC?

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img