30 C
New York

Kocha mpya Liverpool mshahara wake bil. 35/-

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza

LIVERPOOL imemtangaza Andoni Iraola kuwa kocha wake mpya kwa ajili ya msimu ujao, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Arne Slot.

Ripoti zinaeleza kuwa Iraola aliyefanya Bournemouth kuwa moja ya timu tishio kwa vigogo msimu uliomalizika wa 2025-26, amesaini mkataba wa miaka miwili na Liverpool.

Hivyo, atalipwa Pauni milioni 10 (zaidi ya Sh bil. 35 za Tanzania) kwa mwaka, hivyo kuingia kwenye orodha ya makocha wanaovuna pesa ndefu Ligi Kuu ya England (EPL).

Taarifa zinadokeza kuwa kocha huyo ndiye aliyependekeza apewe mkataba mfupi wa miaka miwili, ikielezwa kwamba ndiyo utaratibu wake katika klabu zote alizowahi kuajiriwa.

Klabu ya Liverpool iliamua kumgeukia Iraola baada ya kumkosa Xabi Alonso, ambaye aliwapa kisogo na kujiunga na Chelsea.

Related articles

Recent articles