5.7 C
New York

Familia yahofia Khan amefariki gerezani

Published:

ISLAMABAD, Pakistan

KWA sasa, familia ya Imran Khan inahofia kuwa huenda Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Pakistan amefariki akiwa gerezani. Khan alikuwa Waziri Mkuu kuanzia mwaka 2018 hadi 2022, kabla ya kuondoshwa na Bunge, na kisha kukamatwa mwaka 2013. Anatumikia kifungo cha miaka 14 gerezani kwa makosa ya rushwa.

Hata hivyo, Khan ambaye bado anaungwa mkono na sehemu kubwa ya wananchi, amekuwa akisema mashitaka hayo yametokana na siasa chafu zinazoendelea dhidi yake.

Sasa, dada wa mwanasiasa huyo, Aleema Khan, amesema wasiwasi wao mkubwa juu ya uhai wa Khan unatokana na kitendo cha Serikali kuwazuia kwenda kumtembelea.

Wakati huo huo, Aleema aliweka wazi kuwa mpango wa familia kwa sasa ni kuandaa maandamano makubwa ya nchi nzima kuelekea katika Gereza alilomo Khan. “Tuna wasiwasi mkubwa juu ya afya yake, haki zake za kisheria, na namna kaka yetu anavyoishi gerezani,” alisema Haleema.

Aidha, katika mahojiano yake na DW, aliongeza kuwa mara ya mwisho kwa familia na wanasheria kumuona Imran Khan ilikuwa Oktoba 16, mwaka huu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img