10.7 C
New York

Nyasi zitawaka moto Afcon 2025: Kundi D

Published:

CAIRO, Misri
FAINALI za mwaka huu za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Desemba 21, mwaka huu, na zitafikia ukomo Januari 18, mwakani.
Uchambuzi unaliangazia Kundi D, ambalo linazikutanisha Benin, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Senegal.
Benin watashiriki kwa mara ya tano. Mafanikio makubwa zaidi kwao ni pale walipofika robo fainali katika michuano ya mwaka 2019 baada ya misimu mitatu ya kuishia hatua ya makundi.
Kwa upande wa Botswana, maarufu pia kwa jina la ‘Zebras’, wao hii ni mara yao ya pili kushiriki fainali za AFCON baada ya kuishia makundi katika mashindano ya mwaka 2012.
DRC wako chini ya kocha raia wa Ufaransa, Sebastian Desabre, na hii ni mara yao ya 22 kushiriki michuano hiyo.
Mafanikio makubwa zaidi kwa ‘Leopards’ katika miaka ya hivi karibuni ni kufika nusu fainali msimu uliopita nchini Ivory Coast.
Kuelekea fainali zijazo, isisahaulike kuwa Taifa hilo ni mabingwa mara mbili wa AFCON, wakifanya hivyo katika miaka ya 1968 na 1974.
Senegal, maarufu kwa jina la ‘Lions of Teranga’, ni mabingwa wa AFCON mwaka 2021 na hii itakuwa mara yao ya 18 kushiriki mashindano hayo.
Baada ya ubingwa wa mwaka 2021, msimu uliopita haikuwa mzuri kwa vigogo hao wa soka kwani waliishia hatua ya 16 Bora kwenye mashindano hayo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img