LIMA, Peru
MAHAKAMA Kuu nchini Peru imemuhukumu kifungo cha miaka 11 gerezani rais wa zamani, Pedro Castillo, akituhumiwa kwa uasi.
Mashitaka yaliyokuwa yakimkabili Castillo ni jaribio la kuvunja Bunge ili aongoze kwa misingi ya udikteta mwishoni mwa mwaka 2022.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku moja tu tangu Mahakama ilipomfunga miaka 14 gerezani rais mwingine wa zamani, Martin Vizcarra.
Kwa upande wake, Vizcarra alikuwa na mashitaka ya kupokea rushwa miaka mingi kabla ya kuingia madarakani.
Castillo ali mwaka 2021 na jaribio lake la kuvunja Bunge lilitokana na hofu ya kupigia kura ya kutokuwa na Imani na rais kutokana na tuhuma za rushwa zilizokuwa zikimkabili.
Hata hivyo, mpango wake wa kuvunja Bunge uligonga mwamba baada ya Baraza la Mawaziri kutokumuunga mkono.
Vyombo vya dola vilimkamata akiwa njiani kuelekea katika ubalozi wa Mexico nchini Peru.
Kabla ya hukumu ya miaka 11, waendesha mashitaka walitaka mwanasiasa huyo apewe kifungo cha miaka 34 gerezani.
Published:


