12.7 C
New York

Benki ya Dunia: DRC, Msumbiji zinaongoza kwa umasikini Afrika

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini
UMASIKINI umeendelea kuwa changamoto kubwa kwa Afrika, huku takwimu zikionesha kuwa mamilioni ya watu barani humu wanaishi chini ya Dola tatu kwa siku.
Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia (WB), mataifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Msumbiji na Burundi ni mfano mzuri, ambapo asilimia 80 ya watu wake wanaishi chini ya mstari wa umasikini.
Katika ripoti hiyo, DRC inaongoza barani Afrika na asilimia 85.3 ya watu wake wanaishi kwenye lindi la umasikini.
DRC inakabiliwa na umasikini, licha ya kwamba ni moja ya mataifa yenye utajiri mkubwa wa rasilimali, yakiwamo madini.
Aidha, hali mbaya ya usalama inayochagizwa na vikundi vya waasi, inatajwa kuwa chanzo kikubwa cha kudorora kwa shughuli za kiuchumi nchini humo.
Msumbiji inafuata ikiwa na asilimia 82.2, wakati Malawi na Burundi zinashika nafasi ya tatu na ya nne kwa asilimia 75.4 na 74.2.
Ripoti ya WB inaeleza kuwa zimekuwapo sababu mbalimbali za umasikini katika mataifa ya Afrika ikiwamo kasi ndogo ya maendeleo ya viwanda.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img