WASHINGTON, Marekani
SERIKALI ya Marekani kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Marco Rubio, imeeleza kufikia pazuri katika jitihada za kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine. Hata hivyo, Rubio amesema bado kuna juhudi zinapaswa kufanyika ili kurejesha mahusiano mazuri kati ya nchi Jirani hizo.
Ikulu ya Marekani imetoa taarifa hiyo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Ukraine na wasuluhishi wa Ulaya mjini Geneva, Uswis. Katika hatua nyingine ya mazungumzo hayo, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alionesha kuwa na imani na Marekani akisema walau Rais Donald Trump amekuwa akiwasikiliza.
Kauli hiyo ya Zelensky imekuja baada ya awali Ukraine na washirika wake kuwasilisha malalamiko kuwa jitihada za usuluhishi zimekuwa zikiisikiliza zaidi Urusi katika mazungumzo.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Ikulu ya Marekani, Rubio, amesema mazungumzo ya kupata suluhu ya mgogoro wa mataifa hayo yamekwenda vizuri mjini Geneva.


