18 C
New York

Kuelekea Kombe la Dunia 2026: Ufaransa (29)

Published:

PARIS, Ufaransa
MAARUFU pia kwa jina la ‘Les Blues’, timu ya soka ya taifa ya Ufaransa itashiriki kwa mara ya 17 fainali za Kombe la Dunia. Ufaransa iko nafasi ya tatu kwa ubora duniani.
Ufaransa ni mabingwa mara mbili wa fainali hizo, ambapo walitwaa taji hilo katika miaka ya 1998 na 2018.
Pia, ni mabingwa mara mbili wa fainali za Mataifa ya Ulaya (EURO), wakifanya hivyo katika miaka ya 1984 na 2000.
Kikosi kinanolewa na kiungo wa ulinzi wa zamani wa timu hiyo, Didier Deschamps, ambaye aliajiriwa Julai, 2012.
Deschamps anajivunia kikosi chenye mastaa wengi, wakiwamo Kylian Mbappe (Real Madrid), Ousmane Dembele (PSG) na Michael Olise (Bayern Munich). Mbappe alifunga mabao matano katika mechi za kufuzu.
Kuelekea fainali zijazo, pia kikosi cha Ufaransa kinajivunia uwepo wa Bradley Barcola na Eduardo Camavinga.
Ikumbukwe, Ufaransa haikushiriki fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1994 za Marekani na zile za mwaka 1970 zilizofanyika Mexico. Safari hii, nchi hizo ni wenyeji wa michuano hiyo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img