15 C
New York

Kuelekea Kombe la Dunia 2026: Morocco (21)

Published:

RABAT, Morocco
KWA sasa, Morocco inashika nafasi ya 11 katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
‘Simba wa Atlas’ ni mabingwa mara moja wa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON). Walibeba taji hilo mwaka 1976.
Kocha wa sasa, Walid Regragui, amekuwa kwenye benchi la timu hiyo tangu alipoajiriwa Agosti, 2022.
Kama itakumbukwa, Regragui aliajiriwa miezi michache kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia mwaka 2022, akichukua nafasi ya Vahid Halilhodzic aliyekuwa ameiwezesha kufuzu.
Taifa hilo lina kikosi chenye mastaa wengi wanaocheza barani Ulaya, wakiwamo Ayoub El Kaabi (Olympiacos), Achraf Hakimi (PSG) na Brahim Diaz (Real Madrid). El Kaabi alifunga mabao manne kuisaidia timu hiyo kufuzu.
Morocco waliandika historia mwaka 2022 baada ya kuwa Taifa la kwanza la Afrika kufika nusu fainali tangu Kombe la Dunia lilipoanza mwaka 1930.
Wakitokea Kundi lililokuwa na Canada, Croatia na Ubelgiji, Morocco ilizifunga Hispania na Ureno katika hatua za 16 Bora na robo fainali, kabla ya kutolewa na Ufaransa.
Kwa mara ya kwanza, Morocco imefuzu mara tatu mfululizo kushiriki fainali za Kombe la Dunia. Safari hii, ni kwa ushindi wa mechi zote nane za kuwania tiketi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img