ACCRA, Ghana
NAFASI ya 72 katika viwango vya ubora wa soka vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA). ‘Black Stars’ walikuwa nafasi ya 14 mwaka 2008.
Hao ni mabingwa mara nne wa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON), wakiwa wamefanya hivyo katika miaka ya 1963, 1965, 1978 na 1982.
Kocha mzawa, Otto Addo, ambaye aliajiriwa Machi, mwaka jana, amerejea kwenye benchi la ufundi kwa awamu ya pili.
Addo alikiongoza kikosi hicho katika fainali zilizopita za mwaka 2022 zilizofanyika Qatar lakini alijiuzulu baada ya michuano hiyo kumalizika.
Addo, ambaye alikuwa mchezaji wakati Ghana ilipocheza Kombe la Dunia mwaka 2006, ana kikosi chenye mastaa wengi, wakiwamo Jordan Ayew (Leicester), Mohammed Kudus (Spurs) na Antoine Semenyo (Bournemouth).
Ayew alikuwa silaha muhimu kwenye mechi zao za kuwania tiketi ya kushiriki fainali zijazo za Kombe la Dunia, ambapo mshambuliaji huyo alifunga mabao saba.
Msimu uliopita wa Kombe la Dunia, 2022, Ghana waliishia hatua ya makundi. Kwamba timu hiyo haijavuka makundi katika awamu zote tatu zilizopita za michuano mikubwa (Kombe la Dunia na AFCON).
Mwaka 2010, Ghana ilikaribia kuingia nusu fainali ya Kombe la Dunia, kama si kufungwa kwa penalti na vigogo wa Amerika ya Kusini, Uruguay.
Published:


