19.8 C
New York

Kuelekea Kombe la Dunia 2026: Marekani (5)

Published:

LOS ANGELES, Marekani
TIMU ya soka ya taifa ya Marekani itashiriki fainali za Kombe la Dunia za mwakani ikiwa inashika nafasi ya 14 katika viwango vya ubora wa soka vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Marekani iliwahi kufanya vizuri zaidi katika viwango hivyo ilipopanda hadi nafasi ya nne kwenye viwango hivyo mwaka 2006.
Hii itakuwa mara ya nane kwa timu hiyo kushiriki fainali za Kombe la Dunia baada ya kufanya hivyo katika miaka ya 1991, 2002, 2005, 2007, 2013, 2017 na 2021.
Kocha wa kikosi kwa sasa ni Muargentina aliyewahi kuzinoa Tottenham na PSG, Mauricio Pochettino, ambaye aliajiriwa Septemba, mwaka jana.
Mbali ya uzoefu wa Pochettino, kikosi hicho kina wachezaji wenye majina makubwa, wakiwamo Christian Pulisic (AC Milan), Weston McKennie (Juventus) na Chris Richards (Crystal Palace).
Baada ya kushiriki Kombe la Dunia mara saba mfululizo, Marekani ilizikosa fainali hizo mwaka 2018, kabla ya kurejea mwaka 2022 na kuishia hatua ya mtoano (16 Bora).
Marekani walirejea Kombe la Dunia mwaka 2022 baada ya kuzikosa fainali hizo mwaka 2018.
Msimu ujao, itakuwa ni mara yao ya pili kuwa mwenyeji wa michuano hiyo baada ya kuandaa mwaka 1994, ambapo ilitolewa na Brazil katika hatua ya 16 Bora.
Pochettino anatarajiwa kuwa kocha wa kwanza kuivusha Marekani hatua ya 16 Bora tangu Bruce Arena alipofanya hivyo katika fainali za mwaka 2002.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img