7.8 C
New York

Zelenskyy: Tuko tayari kumaliza vita na Urusi

Published:

KYIV, Ukraine
RAIS wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, amesema Serikali yake iko tayari kushirikiana na Marekani katika jitihada za kumaliza mgogoro na Urusi.
Hivi karibuni, Ikulu ya Marekani ilithibitisha kuwa Rais Donald Trump amepitisha mpango wa kumaliza uhusiano mbaya wa nchi jirani hizo.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Ikulu, Rais Trump amefikia pazuri baada ya mazungumzo yake na Urusi.
Hata hivyo, kile kinachoonekana kuwa bado hakikubaliki kwa upande wa Ukraine, ni kuiachia Urusi iendelee kushikilia baadhi ya maeneo inayoshikilia nchini humo.
Katika hatua nyingine, Mawaziri Wakuu wa nchi za Umoja wa Ulaya (EU) wamekutana kujadili mgogoro kati ya Urusi na Ukraine.
Wakati huo huo, taarifa kutoka kwa viongozi waandamizi wa jeshi nchini Urusi wamedai kuwa vikosi vyao vimeuteka Mji mdogo wa Ukraine, Kupiansk.
Akizungumza na Rais Vladimir Putin, kamanda wa kikosi cha Urusi, Sergei Kuzovlev, aliuita Mji huo kuwa ni ngome ya ulinzi ya Ukraine.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img