7.8 C
New York

Mahakama yamng’oa ofisini Mwanasheria Mkuu

Published:

MADRID, Hispania
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali ya Hispania, Alvaro Garcia Ortiz, ametakiwa na Mahakama Kuu kukaa kando baada ya kukutwa na hatia katika mashitaka ya kuvujisha baadhi ya nyaraka za siri.
Mahakama Kuu imemtaja Garcia Ortiz kuvujisha taarifa za ulipaji kodi za mfanyabiashara Alberto Gonzalez Amador, ambaye ni mpenzi wa mmoja ya wanasiasa maarufu.
Mbali ya kumfungia kujihusisha na nafasi hiyo kwa miaka miwili, pia Mahakama imemtoza faini ya euro 7,200 (zaidi ya Sh mil. 20 za Tanzania)
Wakati huo huo, Garcia Ortiz amelazimishwa na Mahakama kumlipa Gonzalez Amador fidia ya kitita cha euro 10,000.
Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria za Hispania, bado Garcia Ortiz ana haki ya kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama.
Kwa upande mwingine, kilichomkuta kimeelezwa kuwa ni pigo jingine kwa Waziri Mkuu, Pedro Sanchez, ambaye mkewe naye anachunguzwa akihusishwa na ‘unjaujanja’ katika biashara zake.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img