7.8 C
New York

Waziri Mkuu Bangladesh ahukumiwa kifo

Published:

DHAKAN, Bangladesh
ALIYEKUWA Waziri Mkuu wa
Bangladesh, Sheikh Hasina, amehukumiwa kifo kutokana na mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Sheikh Hasina anatajwa kuamrisha vyombo vya dola kutekeleza mauaji wakati wa maandamano yaliyomng’oa madarakani.
Maandamano hayo makubwa yaliyofanyika mwaka jana yaliyoongozwa na wanafunzi yalishuhudia vifo 1,400.
Tangu kung’olewa madarakani Julai, mwaka jana, Hasina amekuwa akiishi uhamishoni nchini India.
Licha ya waendesha mashitaka kumtaja kuwa chanzo cha mauaji, Hasina amekuwa akikana kuhusika na kusema ni kesi ya kisiasa dhidi yake.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img