DOHA, Qatar
SERIKALI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imesaini mkataba wa amani na wapiganaji wa Kundi la waasi la M23 mjini Doha, Qatar.
Ifahamike kuwa makubaliano hayo ni ya kurejesha amani katika maeneo ya Mashariki mwa DRC.
Qatar, kama ilivyo Marekani na Umoja wa Afrika, imekuwa na jitihada za makusudi za kuhakikisha pande mbili hizi zinafikia mwafaka.
Mapema mwaka huu, M23 walitangaza kuiteka Miji miwili mikubwa ya Mashariki, Goma na Bukavu.
Katika makubaliano yaliyofikiwa sasa nchini Qatar, pande mbili hizo zimekubaliana juu ya kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia raia.
M23 wamekuwa wakivutiwa zaidi na usuluhishi unaofanywa na Qatar, ukilinganisha na Marekani na Umoja wa Afrika.
Tangu Januari, mwaka huu, maelfu ya watu wameuawa, huku mamia wakilazimika kuyakimbia makazi yao kutokana na vita kati ya M23 na wanajeshi wa Serikali.
Serikali ya DRC imekuwa ikishutumiwa kugawa madini kwa Marekani ili Taifa hilo kubwa liisaidie katika vita yake na M23.
Wakati huo huo, yapo madai ya muda mrefu, kwamba M23 nao wamekuwa wakisaidiwa na Serikali ya Rwanda chini ya Rais Paul Kagame.
Published:


