10.5 C
New York

Rais Syria aondoshewa vikwazo Umoja wa Mataifa

Published:

NEW YORK, Marekani
BARAZA la Usalama la Umoja wa Mataifa limemuondoshea vikwazo Rais wa Syria, Ahmed al-Sharaa.
Hatua ya kuondoshwa vikwazo inakuja wakati huu Rais huyo akijiandaa kuingia Marekani kwa ajili ya mazungumzo na Donald Trump.
Al-Sharaa anakuwa Rais wa kwanza wa Syria kuitembelea Ikulu ya Marekani tangu nchi hiyo ilipopata uhuru mwaka 1946.
Wakati huo huo, pia Baraza la Usalama limemuondoshea vikwazo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Syria, Anas Khattab.
Kama ilivyo kwa Al-Sharaa, Khattab aliwekewa vikwazo na UN baada ya kuhusishwa na Kundi la kigaidi la Al-Qaeda.
Ikumbukwe, baada ya miaka 13 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, Rais Bashar Assad aliondoshwa madarakani Desemba, mwaka jana.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img