8 C
New York

Wasiojulikana choma moto nyumba ya Polisi Songwe

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

WATU wasiojulikana wamechoma moto nyumba ya Polisi iliyopo Kata ya Chitete, Kijiji cha Ikumbilo, Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, na kuteketeza mali zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 2.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Songwe, Augostino Senga, tukio hilo lilitokea usiku wa Oktoba 22, 2025, wakati mwenye nyumba, Mkaguzi wa Polisi Nsajigwa Mwajeka, akiwa katika majukumu maalum.

Akizungumza leo Ijumaa, Oktoba 24, 2025, Kamanda Senga alisema moto huo uliteketeza vyumba viwili vya nyumba hiyo kabla ya kugunduliwa na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Chitete, Darkson Kamendu.

Amefafanua kuwa miongoni mwa vitu vilivyoharibiwa ni nguo za Kiraia, Sare za Polisi, vyombo vya nyumbani, mahindi, kitanda, godoro na vitu vingine vidogo vidogo.

Kamanda Senga amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa wahalifu walikusanya baadhi ya vitu na kuviweka kitandani, kabla ya kuwasha moto kwa kutumia njiti za kiberiti zilizokutwa eneo la tukio.

Hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo, na Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini wahusika, ambapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa mara watakapotiwa mbaroni.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img