23.5 C
New York

Afrika na safari ya Kombe la Dunia 2026 (2) – Morocco

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini
MATAIFA tisa ya Afrika yameshajihakikishia tiketi ya kushiriki fainali zijazo za Kombe la Dunia za mwakani zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico. Tunisia, Algeria, Ghana, Misri, Senegal, Afrika Kusini, Ivory Coast, Cape Verde na Morocco.
Makala haya yanawaangazia wawakilishi hao wa soka la Afrika kwa kuichambua Morocco. Je, ina nafasi ya kufanya vizuri Kombe la Dunia?
Morocco, kama itakumbukwa, walifanya vizuri katika fainali zilizopita, ambapo waliandika historia ya kuwa timu ya kwanza ya Afrika kufika nusu fainali.
‘Simba wa Atlas’ ilikuwa timu ya kwanza ya Afrika kufuzu fainali zijazo za Kombe la Dunia. Walijihakikishia tiketi yao baada ya ushindi wa mechi sita mfululizo za kufuzu.
Safari yao ya kufuzu ilihitimishwa kwa ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Niger. Kwamba walikata tiketi wakiwa na mechi mbili mkononi na hii inakuwa mara ya tatu mfululizo kwao kwenda Kombe la Dunia.
Morocco bado iko chini ya kocha Walid Regragui aliyeiongoza kufika nusu fainali katika Kombe la Dunia lililopita, inajivunia kikosi chenye wachezaji bora kwa sasa.
Unawazungumzia Achraf Hakimi, Yassine Bounou, Sofyan Amrabat, Youssef En-Nesyri, Brahim Diaz, Hakim Ziyech, Noussair Mazraoui, na Hamza Igamane.
Mwakani itakuwa mara ya saba kwa Morocco kushiriki Kombe la Dunia tangu mwaka 1970, ingawa ni kwa mara ya kwanza kuiona ikishiriki mara tatu mfululizo.

Related articles

Recent articles