24.8 C
New York

Cape Verde yaandika historia kutinga Kombe la Dunia

Published:

PRAIA, Cape Verde
KATIKA historia ya soka, Cape Verde limekuwa taifa dogo la pili kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia. Ni baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Eswatini jana.
Cape Verde iliyopata uhuru mwaka 1975 kutoka kwa Ureno, ni Kisiwa chenye watu wasiozidi 525,000 ni hiyo kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni Benki ya Dunia.
Kabla ya Cape Verde, Iceland ndilo taifa dogo zaidi kuwahi kushiriki Kombe la Dunia. Ilifanya hivyo mwaka 2018.
Jana, Rais wa Cape Verde, Jose Maria Neves, alikuwa miongoni mwa mashabiki waliokuwa uwanjani kuishuhudia timu yao ikifuzu.
Kwa miaka ya hivi karibuni, Taifa hilo limekuwa na maendeleo makubwa, hasa kwenye michuano ya fainali za Mataifa Afrika (AFCON).
Ikishiriki kwa mara ya kwanza mwaka 2013, Cape Verde iliweza kufika robo fainali, kabla ya kurudia maajabu hayo mwaka 2023.
Ni kutokana na maendeleo hayo, sasa inashika nafasi ya 70 katika viwango vya ubora wa soka vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Related articles

Recent articles