23.3 C
New York

Wanajeshi Israel waanza kuondoka Gaza

Published:

JERUSALEM, Palestina
KATIKA kile kinachotafsiriwa kuwa ni hatua nzuri katika kumaliza mgogoro wa Gaza, wanajeshi wa Israel wameanza kuondoka katika Ukanda huo.
Kurejea nyumbani kwa wanajeshi wa Israel ni sehemu ya makubaliano ya kumaliza vita kati ya nchi hiyo na wapiganaji wa Hamas.
Hata hivyo, walioondoka ni baadhi tu ya wanajeshi lakini bado Israel inaendelea kushikilia baadhi ya maeneo ya Ukanda wa Gaza.
Katika picha za video zilizosambaa, maelfu ya raia wa Palestina wanaonekana wakirejea Kaskazini mwa Gaza, eneo ambalo lilikuwa chini ya vikosi vya Israel kwa miezi ya hivi karibuni.
Ikiwa ni sehemu ya makubaliano, Hamas wanatakiwa kuachia mateka takribani 28 wa Israel kufikia Jumatatu ya wiki ijayo.
Pia, Israel italazimika kuachia raia 250 wa Palestina inaowashikilia katika magereza yao wakitumikia vifungo vya maisha.

Related articles

Recent articles