20.9 C
New York

Aubameyang afunga manne, alimwa nyekundu

Published:

BANJUI, Gambia
KATIKA mchezo wa jana, straika Pierre-Emerick Aubameyang alifunga mabao yote katika ushindi wa 4-3 wa timu yake ya taifa ya Gabon dhidi ya Gambia.
Ushindi huo umeifanya Gambia kuzidiwa pointi moja tu na Ivory Coast iliyojichimbia kileleni mwa Kundi F, huku timu moja tu ikiwa na nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwakani.
Zikiwa zimebaki dakika tano tu kabla ya mchezo kuisha, nyota huyo wa zamani wa Arsenal alilimwa kadi nyekundu baada ya kadi ya njano ya pili kwa kitendo chake cha kumsukuma beki wa Gambia, Alagie Saine.
Awali, alishapata kadi ya kwanza ya njano kutokana na kitendo chake cha kupiga teke na kuvunja kibendera wakati akishangilia bao lake la nne.
Ni kutokana na adhabu hiyo sasa, Aubameyang ataikosa mechi ya mwisho ya kufuzu, wakati Gabon itakapokuwa nyumbani kumenyana na Burundi mapema wiki ijayo.
Mbaya zaidi, ili Gabon ifuzu moja kwa moja, italazimika kupata ushindi na kuiombea Ivory Coast ipoteze ikiwa nyumbani dhidi ya Kenya.

Related articles

Recent articles